KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amekanusha uvumi ulioenea katika mitandao ya
jamii kuhusu kukamatwa magaidi
mkoani Arusha usiku wa kuamkia
leo waliokuwa wamejitayarisha kukishambulia Chuo cha Uhasibu (Institute of
Accountancy Arusha - IAA) wakidaiwa kuwa na gari
aina ya Toyota Premio nyeusi
ikiwa na watu wanne na bunduki nne aina ya SMG na risasi 160 walipojaribu
kuingia chuoni hapo.
Inadaiwa katika taaifa hiyo isiyojulikana chanzo chake
kwamba watu hao walijifanya ndugu wa
mwanafunzi mmoja wa kike anayeishi kwenye hosteli zilizo ndani ya chuo hicho.
Rais wa chuo hicho, Iman Mkumbo, naye amesema
habari hizo hazina ukweli wowote.
No comments:
Post a Comment