Cameron Diaz.
NIjambo
la kuhuzunisha kwa mwanamke aliyekamilika kutokuwa na mtoto katika
kipindi cha maisha yake, hii inatokana na ukweli kwamba watoto ni chanzo
kikubwa cha furaha kwa wazazi hasa wa kike bila kujali hadhi waliyonayo
katika jamii.
Familia nyingi hasa wanawake wamejikuta katika wakati mgumu kutokana na masimango kutoka kwa jamii na watu wanaowazunguka huku matatizo hayo yakiwajumuisha pia mastaa kama Wema Sepetu, Jacqueline Wolper, Lady Jaydee, Johari, Maya na wengine wengi ambao wanatamani lakini hawajabahatika kuwa na watoto.

Makala haya yanaonesha jinsi hali hiyo ya kukatisha tamaa
inavyowakumba hata mastaa wakubwa wa majuu ambao umri unayoyoma bila
kujaaliwa kupata watoto lakini wamejijenga kisaikolojia na kuichukulia
hali hiyo kama suala la kawaida .
Janet Jackson.
Janet Jackson (49)
Ni mwanamuziki na mwanamitindo
mwenye mvuto kutoka familia yenye vipaji ya ‘Jackson.’ Pamoja na
kuolewa mara kadhaa
hajawahi kupata mtoto. Taarifa zilizopo zinadai kuwa Janet hapendi kuzaa kwa kuhofia kuharibu umbile lake, lakini sababu hiyo inapingwa vikali na watu mbalimbali wanaodai kuwa ni mgumba.
hajawahi kupata mtoto. Taarifa zilizopo zinadai kuwa Janet hapendi kuzaa kwa kuhofia kuharibu umbile lake, lakini sababu hiyo inapingwa vikali na watu mbalimbali wanaodai kuwa ni mgumba.
Cameron Diaz (43)
Huyu ni mkali wa filamu kutoka
Marekani ambaye hajawahi kuolewa wala kuwa na mtoto. Katika mahojiano
yake na vyombo mbalimbali vya habari, alidai kuwa anafurahia hali hiyo
ya kuwa peke yake na kuongeza kuwa watoto siyo chanzo cha furaha pekee
kwa mwan-amke bali kuna vitu vingine zaidi.
Oprah Winfrey.
Oprah Winfrey (61 )
Anatajwa kama mwanamke tajiri
mkubwa duniani ambapo akiwa katika umri wa miaka 14 alipata ujauzito
baada ya kubakwa. Aliwahi kusimulia kuwa alilazimika kunywa ‘blichi’ ili
kutoa ujauzito huo ambao baba yake aliuita kama aibu kwa familia yao.
Kwa bahati mbaya mimba iliharibika na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa
hajawahi kuolewa wala kupata mtoto.
Tyra Banks (42)
Ni mwanamitindo wa kiwango cha
juu kutoka Marekani, ambaye alishawahi kutoka kimapenzi na mastaa kibao
wa kiume kama vile, Justin Timberlake na Seal, pamoja na kutoka na
mastaa hao lakini hajawahi kuwa na mtoto.
No comments:
Post a Comment