Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 15, 2015

UMRI UMEWATUPA NA HAWANA WATOTO


Cameron Diaz.
NIjambo la kuhuzunisha kwa mwanamke aliyekamilika kutokuwa na mtoto katika kipindi cha maisha yake, hii inatokana na ukweli kwamba watoto ni chanzo kikubwa cha furaha kwa wazazi hasa wa kike bila kujali hadhi waliyonayo katika jamii.
Familia nyingi hasa wanawake wamejikuta katika wakati mgumu kutokana na masimango kutoka kwa jamii na watu wanaowazunguka huku matatizo hayo yakiwajumuisha pia mastaa kama Wema Sepetu, Jacqueline Wolper, Lady Jaydee, Johari, Maya na wengine wengi ambao wanatamani lakini hawajabahatika kuwa na watoto.
Makala haya yanaonesha jinsi hali hiyo ya kukatisha tamaa inavyowakumba hata mastaa wakubwa wa majuu ambao umri unayoyoma bila kujaaliwa kupata watoto lakini wamejijenga kisaikolojia na kuichukulia hali hiyo kama suala la kawaida .
Janet Jackson.
Janet Jackson (49)
Ni mwanamuziki na mwanamitindo mwenye mvuto kutoka familia yenye vipaji ya ‘Jackson.’ Pamoja na kuolewa mara kadhaa 


hajawahi kupata mtoto. Taarifa zilizopo zinadai kuwa Janet hapendi kuzaa kwa kuhofia kuharibu umbile lake, lakini sababu hiyo inapingwa vikali na watu mbalimbali wanaodai kuwa ni mgumba.
Cameron Diaz (43)
Huyu ni mkali wa filamu kutoka Marekani ambaye hajawahi kuolewa wala kuwa na mtoto. Katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari, alidai kuwa anafurahia hali hiyo ya kuwa peke yake na kuongeza kuwa watoto siyo chanzo cha furaha pekee kwa mwan-amke bali kuna vitu vingine zaidi.
Oprah Winfrey.
Oprah Winfrey (61 )
Anatajwa kama mwanamke tajiri mkubwa duniani ambapo akiwa katika umri wa miaka 14 alipata ujauzito baada ya kubakwa. Aliwahi kusimulia kuwa alilazimika kunywa ‘blichi’ ili kutoa ujauzito huo ambao baba yake aliuita kama aibu kwa familia yao. Kwa bahati mbaya mimba iliharibika na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa hajawahi kuolewa wala kupata mtoto.
Tyra Banks (42)
Ni mwanamitindo wa kiwango cha juu kutoka Marekani, ambaye alishawahi kutoka kimapenzi na mastaa kibao wa kiume kama vile, Justin Timberlake na Seal, pamoja na kutoka na mastaa hao lakini hajawahi kuwa na mtoto.

No comments:

Post a Comment