Pages

Thursday, April 16, 2015

WAZIRI KIVULI WA ELIMU APINGA SERIKALI KUWATAKA WALIMU KUJIELEZA KWA WAKUU WA MIKOA

Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Suzan Lyimo (Chadema) akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo, kuhusu matatizo katika sekta ya elimu. Kushoto ni Katibu wa Bawacha, Grace Tendega. (Picha na Francis Dande)

Na MwandishiWetu

WAZIRI kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Suzan Lymo, amepinga kitendo cha serikali cha kuwataka walimu waliofunga shule kutokana na uhaba wa chakula waende wakajieleze kwa Mkuu wa Mkoa kutokana na hatua hiyo.


Suzan, alitoa kauli hiyo baada ya serikali kudai kuwa tayari ilikuwa imekwishapeleka fedha hivyo walimu hao hawakupaswa kufanya hivyo.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri huyo kivuli, alisema jambo hilo halishangazi kwa vile inaeleweka kuwa serikali legelege huzaa maamuzi mabovu yasiyo na mantiki.

“Cha ajabu leo hii watoto wanarudishwa nyumbani au kucheleweshwa kutofungua shule baada ya likizo ya Pasaka, kwa kuwa wazabuni hajalipwa fedha zao na hivyo hawawe kununua vyakula tena,”alisema Zuzan.

Alisema, hatua za walimu kuwarudisha nyumbani wanafunzi, zilikuwa sahihi kwani kama wangewaacha shuleni hapo huku kukiwa hakuna chakula ieleweke wazi kuwa wanafunzi hao wangefanya vurugu ambazo zingeweza kuleta matatizo mengine.

“Nawapongeza walimu wakuu kwa utaratibu huo swali ni je walimu wanajua kiasi cha fedha wanachopaswa kupewa?

“Hii ni aibu kubwa kwa serikali, kama mdau wa elimu imenisikitisha sana na ninatambua kuwa baadhi ya wazabuni ni wazalendo na wengine hata wanakopa kwa ajili ya kulisha wanafunzi hawa lakini wamefika ukomo,”alisema Suzan.

Suzan, alisema kuwa mwezi wa tano ni wa mitihani ya kidato cha sita hivyo wanafunzi wanapaswa kusoma kwa bidii bila bugudha ili waweze kufanya vizuri.

 “Nashangaa baadala ya kufanya hivyo wanavurugwa huku wenzao washule binafsi wakiendelea na masomo sasa kutokana na wanafunzi hao kupoteza vipindi matokeo yake ni wanafunzi kufeli mitihani,”alisema Suzan.


Hata hivyo, alishangazwa kusikia kuwa hadi sasa ni asilimia 62 ya fedha za kulisha shule zimetolewa wakati hii ni robo ya mwisho wa mwaka, ambapo ilitakiwa kufikia kipindi hiki iwe ilipswa asilimia 75 zimekwisha lipwa.

No comments:

Post a Comment