Pages

Thursday, May 28, 2015

MAAFISA SABA WA JUU WA FIFA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA MJINI ZURICH NCHINI SWITZERLAND



Maafisa saba wa juu wa shirikisho la soka duniani, FIFA wamekamatwa kwa shutuma za kupokea rushwa. Maafisa hao walikamatwa kwenye hoteli ya Baur au Lac ya jijini Zurich, Jumatano hii. Polisi wa Uswisi wamekamata maafisa hao wakiwemo makamu wa rais wawili baada ya kuivamia kwa kushtukiza hoteli hiyo.
 Makamu wa rais wa FIFA, Jeffrey Webb anaaminika kuwa mmoja wa maafisa waliokamatwa alfajiri ya leo wakiwa kwenye hoteli ya kifahari nchini Uswisi.
 
Eduardo Li, kutoka Costa Rica naye pia alikamatwa kwenye hoteli hiyo ya kifahari 
Hatua hiyo imekuja kufuatia upelelezi uliofanywa na Marekani kwa kipindi cha miaka mitatu. Waendesha mashtaka wa Marekani wametoa hati za kukamatwa kwa maofisa 14, kwa madai yakiwemo kutakatisha fedha haramu, ulaghai na mengine.
Madai hayo ni pamoja na maafisa wa FIFA kupokea rushwa ifikayo dola milioni 150.
Mamlaka za Uswisi zimefungua upelelezi tofauti wa jinai katika utendaji wa FIFA kuhusiana na nafasi za kuandaa makombe ya dunia ya mwaka 2018 na 2022 zilizoenda kwa Urusi na Qatar.


Rais wa FIFA Sepp Blatter si miongoni mwa wanaoshtakiwa lakini alikuwa mmoja wa maafisa waliokuwa wakichunguzwa.

Uchaguzi wa FIFA utaendelea kama ulivyopangwa Ijumaa hii na pia michuano ya kombe la dunia nchini Urusi na Qatar haitaathirika.

No comments:

Post a Comment