Pages

Thursday, May 28, 2015

RAIS KIKWETE AMWAPISHA KATIBU MKUU MAMBO YA NJE NA NAIBU WAKE


mul2
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Balozi Liberate Mulamula akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.
mul3
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Balozi liberate Mulamula akipokea vitendea kazi kutoka kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.
mul4
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Balozi Hassan Simba Yahya akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.


mul5
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Balozi Hassan Simba Yahya akipokea vitendea kazi kutoka kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.
mul6
Balozi mpya wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mh.Hemed Iddi Mgaza akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa miongozo ya kazi.
 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa na Naibu wake pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Saudi Arabia katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.

                   ( Picha na Freddy Maro )

No comments:

Post a Comment