MWAKILISHI viti maalumu wanawake CUF wilaya ya
Chake Chake, Mhe. Salma Mohamed Ali (kulia) akimkabidhi dawa na vifaa tiba, Daktari dhamana wa hospitali ya Chake Chake, Dk. Yussufu Hamad Idd
vilivyotolewa na mwakilishi wa Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali
Shehe, Mei 3 mwaka huu, kabla ya baadhi ya vifaa na dawa hizo
kugunduilika kupitiwa na muda wake wa matumizi.
BAADHI ya dawa na vifaa tiba zilizotolewa hivi
karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe
ambazo tayari zimeshapitiwa na muda wake wa matumizi, ambapo uongozi wa hospitali ya Chake chake
umezigundua wakati wakitaka kuzitumia.
MFAMASIA mkuu wa hospitali ya Chake Chake Pemba, Dk. Kassim Zahir akionyesha vipamba vya kusafisa damu baada ya
kung’olewa jino, ambavyo navyo ni miongoni mwa vifaa tiba
vilivyogundulika kupitiwa na muda wake, ambavyo
vilitolewa hivi karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe, pamoja na dawa nyengine.
DAKTARI dhamana wa hospital ya Chake Chake Pemba, Dk. Yussuf Hamad Idd, akitoa maelezo jinsi watakavyomkabidhi dawa na
vifaa tiba Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali Shehe ambaye hivi karibuni alikabidhi dawa hizo ambazo zimegundulika
kupitwa na muda wake wa matumizi.(Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment