Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 3, 2015

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AZINDUA DUKA JIPYA LA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA TIGO.‏

Duka jipya la kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi,Tigo lafunguliwa mjini Moshi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka jipya la kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.wengine wanaoshuhudia toka kulia ni mkuu wa 



wilaya ya Moshi,Novatus Makunga,Meneja huduma kwa wateja kanda ya kaskazini,Gwamaka Mwakilembe na kushoto ni Meneneja wa Ubora wa Huduma ka wateja ,Mwangaza Matotola.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya simu za mkononi ya Tigo lililozinduliwa mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akifuatilia kwa makini shughuli za uzinduzi wa duka la Tigo katika mji wa Moshi.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo,wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo mjini Moshi.
Meneja huduma kwa wateja kanda ya Kaskazini,Gwamaka Mwakilembe akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea vitengo mbalimbali ndani ya duka hilo.
Wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakiwa kazini.
Uuzaji wa simu za aina mbalimbali pia ulikuwa ukifanyika katika duka hilo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama ,akifurahia jambo mara baada ya kutembelea ndani ya duka hilo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ya Tigo.
Meneja huduma kwa wateja Kanda ya Kaskazini,Gwamaka Mwakilembe akitoa neno la shukurani kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama (hayupo pichani)mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya Tigo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo muda mfupi mara baada ya uzinduzi wa duka hilo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment