Kutokana
na hali hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imemwomba Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuzuia mchakato
wowote haramu utakaofanywa na Gama kuhusu ardhi.
RC
Gama, alitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Halima Mdee (Chadema) wakati akiwasilisha maoni ya Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2015/16
mjini Dodoma jana.
Alisema
Gama anashirikiana na kampuni binafsi ya Jun Yu Investment
International, anataka kumiliki ardhi iliyokwishalipiwa fidia ya Sh
milioni 168 na Halmashauri ya Wilaya ya Rombo jambo ambalo ni kinyume
cha sheria.
Mdee
ambaye pia ni Mbunge wa Kawe jijni Dar es Salaam, katika hotuba yake,
aliambatanisha vielelezo vinavyomwonyesha Gama kuhusika katika kampuni
hiyo.
Aliwataja
wahusika wengine kuwa ni Wang Zhigang raia wa China anayemiliki hisa
48,000, Feng Hu raia China mwenye hisa 49 na Muyanga Leonidas Gama
ambaye ni mtoto wa Gama anayemiliki hisa 3,000.
“Habari
tulizonazo, mkuu wa mkoa anamiliki hisa 20,000 ambapo hisa 10,000
zimefichwa kwa mwanahisa wa kwanza na 10,000 nyingine kwa mwanahisa wa
pili kupitia mkataba wa pili uliofichwa, ambao pia tumeuambatanisha
katika hotuba hii.
“Katika
hali ya kushangaza, Halmashauri ya Rombo ambayo iliwekeza fedha zake Sh
milioni 168 haitambuliwi na wala haina hisa hata moja katika kampuni
hiyo,” alisema Mdee.
Alisema
kambi ya upinzani ina taarifa za kiintelijensia ambazo zinaonyesha
wawekezaji hao wa kichina walilipa Sh milioni 500 kama fidia kwa
wananchi katika ardhi hiyo ambayo Halmashauri ya Rombo ilishalipa Sh
milioni 168, lakini fedha hizo hazijulikani zilipo.
Mdee,
pia alimtaja Gama kutaka kufanya ufisadi katika eneo lililopo
Kilalacha ambalo linagusa Jimbo la Vunjo na Rombo lenye ukubwa wa hekta
2,700.
Akizungumzia
suala hilo, Mdee alisema eneo hilo lilikuwa mali ya ushirika uliokuwa
ukifahamika kwa jina la Lokolova, lakini katika siku za karibuni kigogo
huyo wa mkoa amekuwa akilinyemelemea kwa kisingizio cha uwekezaji.
Alisema
Gama yupo nyuma ya mgogoro wa ardhi unaokihusisha kiwanja cha Mawenzi
chenye hati namba C.T 056035 kilichokuwa chini ya miliki ya The
Registered Trustees of Mawenzi Sport Club.
“Kiwanja
hiki kilikuwa na hatimiliki ya miaka 33 iliyokwisha mwaka 1974. Mwaka
1994 kupitia kwa aliyekuwa waziri wa ardhi wakati huo, Edward Lowassa,
alitoa amri ya kutwaa maeneo mbalimbali likiwamo hilo.
“Hali
ilikuwa salama kwa wakuu wote wa mikoa waliopita, lakini hali
ilibadilika alipoletwa Gama ambaye amekuwa akitumia ofisi yake
kushinikiza kiwanja husika kikabidhiwe kwa matapeli ambao wametengeneza
nyaraka feki na kuziwasilisha kwa Wakala wa Udhamini na Ufilisi (RITA)
na kujitambulisha kama wadhamini wapya baada ya kukabidhiwa na wadhamini
wa awali.
“Wakati
matapeli hawa wanaotambulika kwa majina ya Amratlal N. Pattn na Hittesh
H. Solan wakionyesha kikao cha makabidhiano kilifanyika Januari 5, 2008
mbele ya wadhamini wa awali, Devchad Nathu Shah na Mohamedal Sharriff,
taarifa za uhakika ni kwamba Shah alishafariki dunia tangu mwaka 1979
wakati Sharriff alifariki mwaka 1998,” alisema Mdee.
Awali
akitoa hotuba ya makadirio ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016, Waziri
Lukuvi alionya makundi yanayochukua ardhi ya wananchi kwa ajili ya
matumizi mbalimbali kutokulipa fidia kwa mujibu wa sheria.
Alisema
watumishi wa sekta ya ardhi, watakaobainika kusababisha kero kwa
wananchi, hususan katika halmashauri nchini, watachukuliwa hatua ikiwamo
kufukuzwa kazi.
No comments:
Post a Comment