Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, June 11, 2015

URAIS 2015 WASANII WAGAWANYIKA VIPANDE WENGINE KWA LOWASA NA WENGINE MEMBE

Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe.
MPASUKO! Zikiwa zimesalia takriban siku 31 kabla ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpitisha mgombea mmoja wa urais atakayechuana na vyama vya upinzani, imebainika kuwa mastaa wa filamu na Bongo Fleva wamegawanyika vipande huku wakiwa kwenye msuguano mkali kufanikisha ushindi wa makada Bernard Membe na Edward Lowassa, 

 
Risasi Mchanganyiko linapa mchapo kamili.
WAJIPAMBANUA
Taarifa kutoka ndani ya tasnia hizo ambazo zina nguvu ya ushawishi katika jamii zimeeleza kuwa, Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwa kiwango kikubwa amewakamata wasanii wengi wa Bongo Movies wanaomuunga mkono huku Lowassa (Waziri Mkuu wa zamani) akiwa amewadhibiti vilivyo mastaa wa Bongo Fleva.
“Ni mpasuko wa aina yake, Membe ameonekana kuwakamata kisawasawa wasanii wa Bongo Movies na ndiyo maana hata juzi (Jumapili iliyopita), mastaa wengi wa filamu walikwenda Lindi kumuunga mkono alipokuwa anatangaza nia.

No comments:

Post a Comment