Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 1, 2015

PICHA::NAY WA MITEGO: Sitaki Watoto Wangu Wasome kwa Shida Ndiyo Maana Nimewanunulia Gari la Kuwapeleka Shule.

Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amefunguka kuwa hataki watoto wake,Curtis na Munie wasome kwa shida kama yeye alivyosoma kwa tabu,ndiyo maana amewanunulia gari la kuwapeleka shule.

Akipiga stori na Clouds FM,alisema kuwa gari hilo lina vitu muhimu ndani kama meza ya kulia chakula,sinki la kunawia mikono,kitanda cha kulalia,TV na huduma nyingine ambalo wataanza kulitumia mwakani.
‘’Unajua mimi nilisoma kwa shida sana,sasa sitaki watoto wangu wapate shida ndiyo maana 

 
nimewanunulia gari la kuwapeleka shule wataanza kulitumia mwakani,na nitaajiri dereva wa kuwapeleka shule,’alisema Nay

No comments:

Post a Comment