New York, Marekani
IMETULIA! Marafiki North West na Penelope Disick, 3, ambao
ni watoto wa wanandugu, Kim na Kourtney Kardashian wamezidi kuonyesha kiwango
kikubwa cha upendo kati yao lakini kubwa ni kwamba sasa umezidi.
North West na Penelope Disick wakifurahia jambo.
Mtandao mmoja wa habari za burudani za mastaa wa nje uliwapa
shavu watoto hao licha ya kuwa na umri mdogo lakini wanaonyesha kuwa ni
marafiki wakubwa kuanzia nyumbani hadi katika mitoko wanapokuwa na mama zao.
Awali wakiwa wadogo zaidi, mama zao walikuwa wakiwapiga
picha na kutupia kwenye mitandao ya kijamii na kuandika ‘marafiki’ lakini hilo
ni kama waliwatabiria kwani sasa ni ‘mabesti’ walioshibana.
Licha ya kuwa Penelope ana kaka yake ambaye ni Mason Dash,
5, na mdogo wao Reign, wala hajaonyesha urafiki dhidi yao kama ule alionao na
North huku upendo baina yao ukifananishwa na ule wa akina dada wa Kardashian na
Jenner.
Katika mitoko yao mingi, North amekuwa akionekana kuwa
karibu zaidi na Penelope kuliko mama yake na wakati mwingine wamekuwa wakivaa
sare.
Wikiendi iliyopita mtandao huo wa kiburudani uliwauliza
mashabiki wake kuhusiana na urafiki baina ya North na Penelope ambapo 89.55%
waliupongeza na 10.45 waliona kawaida.
No comments:
Post a Comment