Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Hamad Masauni akizindua michuano ya Bonaza la Kombe la Masauni, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku na kushirikisha timu mbalimbali za vijana ili kukuza vipaji vya mchezo huo Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa Bonaza la Kombe la Masauni yanayofanyika usiku katika viwanja vya malindi mnazi mmoja.
Kikosi cha timu ya Kisimajongoo kinachoshiriki Bonaza la Kombe la Masauni wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wawa ufunguzi uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku. timu hii imeshinda katika mchezo huo 2--1
Kikosi cha timu ya Kikwajuni Bondeni kilichokubali kipigo cha mabao 2--1 dhidi ya timu ya Kisimajongoo.
Wapenzi wa mchezo wa mpira wakifuatilia michezo wa Bonaza ya Kombe la Masauni yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Kocha wa timu ya Kisimajongoo akitowa maelezo kwa wachezaji wa timu yake ikiwa tayari iko mbele kwa mabao 2--1
Kocha wa Timu ya Kikwajuni Bondeni akitowa maelekezo kwa wachezaji wa timu yake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji wa timu ya Kisimajongoo na Kikwajuni Bondeni wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Bonaza la Kombe la Masauni Zanzibar.
Kizaaza golini kwa timu ya Kisimajongoo wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Bonaza la Kombe la Masauni, yanayofanyika usiku katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar.
No comments:
Post a Comment