Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, August 2, 2015

LOWASSA AREJESHA FOMU YA KUWANIA URAIS 2015 KUPITIA UKAWA


 WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, akipungia wafuasi wa CHADEMA na wananchi wengine waliofurika makao makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam,  Jumamosi Agosti 1, 2015, baada ya kurejesha fomu za kukiomba chama chake kumteua kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ndiye atakayesimama kwa niaba ya vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.
 Mh. Lowassa, akikabidhi fomu hizo, kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Tanzania Bara), Profesa Abdallah Safari
 Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Kanda 10 za CHADEMA, Benson Kigaila, akionyesha lundo la fomu zilizomdhamini Mh. Lowassa

 
 Mh. Lowassa, akipongezwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya chama hicho, Mabere Nyaucho Marando.
 Wabunge wa CHADEMA na majimbo yao kwenye mabano kutoka kushoto, Godbless Lema (Arusha Mjini), Wenje (Nyamagana), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
 Mh. Lowassa, akiwa na Esther Bulaya.
 Wabunge na viongozi wa CHADEMA.

No comments:

Post a Comment