Muigizaji na muongozaji wa filamu, Jacob Stephen aka JB amesema amesikitishwa na mfumo wa elimu ya Tanzania baada ya kushindwa kumpata mtanzania wa kushika nafasi ya masoko kwenye kampuni yake mpya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, JB amesema ni Mkenya pekee ndiye aliyeonesha uwezo mzuri na hivyo kupewa kazi hiyo.
Haya ndio aliyoandika:
Jana nimesikitika sana…kuna kampuni mpya ambayo na mimi nina hisa zangu chache na wazungu fulani (nitaitangaza baadae) ilikuwa inataka watu wa
masoko…dah mmh watu karibu 10 kwenye usahili. Wana madigree yao hawana mbinu mpya za kuingiza bidhaa hiyo sokoni, kaja mkenya kashinda, hivi elimu yetu inatuandaa kuwa tutakapomaliza tuwe chini ya mabosi tutakao wakuta kazini.elimu gani hiyo inashindwa kuikomboa jamii inayokuzunguka. elimu isiyoweza kuajiri hata watu 5. angalia hata kwenye fani zetu uigizaji,mziki,watangazaji hata waandishi wasomi wengi hawapo na watu wanafanya vizuri. ingawa sasa tunahitaji mbinu mpya toka kwao. mzungu alichukia akasema machinga wana mbinu mpya kuliko hawa…akosee mtu kizungu utawaona heee wasanii hawajasoma…jiulize elimu yako imelisaidia nn taifa. sisi wengi wetu ni form4 lakini tumetoa ajira kubwa kwa watu. wasanii,liabrary,machinga,maduka mengi tu ingawa tuna mapungufu mengi. wasomi njooni tusaidiane huku pia kuna pesa amkeni. Maandishi na Bongo 5
No comments:
Post a Comment