Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 17, 2015

WAZAZI MATINEJA WAHITIMU ELIMU MBADALA‏

IMG_1858
Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kulia) akipokea kitabu cha wageni kutoka kwa Mratibu wa kata ya Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Bi. Victoria Maige alipofikia katika ofisi hizo kwa ajili ya zoezi la kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAZAZI wenye umri mdogo 149 mkoani Shinyanga ambao walipata mimba wakiwa shuleni wamekamilisha mafunzo ya miaka miwili ya stadi mbalimbali za maisha mkoani hapa.
Wazazi hao wenye umri mdogo ni miongoni mwa wazazi 220 walioanza mafunzo hayo miaka miwili iliyopita chini ya mradi wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhiliwa na Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Wazazi hao vijana kutoka wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga za halmashauri ya Shinyanga, Msalala na Kahama walikuwa wanajifunza katika vituo 10.
Wengine walishindwa kuhitimisha mafunzo yao kwa sababu tofauti.
Pamoja na kumaliza mafunzo hayo na wengine kujiandaa kwa masomo ya sekondari, wanafunzi hao walijifunza shughuli mbalimbali ambazo zinawawezesha kujiajiri na kuongeza kipato kwa familia zao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Msalala, Vivian Masangya alisema pamoja na akimama wadogo hao wengine walishindwa kukamilisha masomo yao kutokana na utoro uliosababishwa na familia, umbali wa vituo husika na wawezeshaji kuwa na posho ndogo ya kuwezesha mafunzo kumekuwepo na mafanikio makubwa.
IMG_1872
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za kata ya Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko na kushoto ni Mratibu wa kata ya Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Bi. Victoria Maige.
Alisema pamoja na changamoto hizo mradi huo umesaidia kurejesha heshima na uwezo wa akina mama hao wadogo na kuonesha njia kwa wengine ambao wamejikuta katika mazingira kama ya hao waliohitimu.
Alisema mila potofu za kuozesha mabinti wadogo na kuwabebea majukumu ya uzazi wakiwa wadogo na kisha wengine kukimbiwa na wale waliowapa ujauzito amefurahishwa sana kuona kwamba waliobaki wamehitimu kwa kishindo.
 
Naye Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta , akimwakilisha Mkuu wa Ofisi ya UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema amefurahishwa na kukamilika kwa mradi huo ambao ulipokea dola 400,000 kutoka kwa serikali ya Japan.
Alisema mradi huo umetokana na mahitaji ya Tanzania katika kukabiliana na tatizo la elimu kwa wasichana wanaokatishwa ndoto zao kwa kupata ujauzito au kuolewa wakiwa wadogo.
“kama Unesco hatuna mradi. Mradi unakuwa wa serikali wanaeleza tatizo tunakaa pamoja tunaliangalia na kuona namna ya kulitatua” alisema Kotta wakati akisema ubunifu wa mradi huo ambao ulikuwa na lengo la kusaidia wasichana kufikia usawa wa jinsia kwa kuwa ukimwezesha kielimu mtoto wa kike utakuwa umeelimisha familia na mwisho taifa.
IMG_1895
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta (kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila alipowasili kwenye ukumbi yalipofanyika mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Aliwataka wahitimu kutoacha kuyatumia mafunzo yao kwa kuwa tayari wamekuwa na msingi sasa wanaweza kusonga mbele katika kusaka elimu.
Alisema wameshapata elimu ya kujitambua na wanachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba hawabaki nyuma katika jamii yao.
“..Tumefunguliwa njia na sasa ni lazima hatua nyingine kufikia ustawi… tukaze mwendo kwa kutumia taasisi za elimu ili kufikia ndoto zetu za kielimu” alisema Kotta.
Naye Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Dk. Noriko Tanaka akizungumza kwa niaba ya balozi wake alisema kwamba serikali ya Japan imefurahishwa na jinsi msaada wake ulivyotumika kuwawezesha akina wadogo kujitambua na kutengeneza mustakabali wa maisha yao.
Alisema katika hotuba yake kwamba anaamini wanawake hao wataanza maisha mapya baada ya kuhitimu na kuonesha tofauti ambayo itasaidia kuwajenga wao kifamilia na kiuchumi.
IMG_1914
Meza kuu katika mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Alisema dola 400,000 zilizotolewa kupitia Mfuko wa Pamoja wa Japan na Unesco ni sehemu tu ya juhudi za Japan kusaidia wale waliokwamishwa katika maendeleo yao kwa sababu mbalimbali waweze kujitambua na kushiriki katika kujiendeleza na kuendeleza taifa.
Aidha alisema katika juhudi hizo hizo hivi karibuni walifungua hosteli ya wasichana ambayo wanaamini itasaidia kuondoa tatizo la wasichana wa shule kukaa na kuwakwepesha na mimba zisizoza lazima.
Alisema ni lengo la ubalozi wake kuhakikisha wanawawezesha wasichana kuwa na nafasi sawa kielimu katika kuambatana na malengo ya millennia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Julius Mlongo, Juni mwaka huu alisema kwamba takwimu zinaonesha kwamba Shinyanga inaoongoza kwa mimba za utotoni nchini.
Alisema hali hiyo inatokana na wazazi wengi kushindwa kuwahimiza mabinti zao kwenda shule.
Takwimu duniani zinaonesha kwamba wanawake milioni 400 wenye umri wa miaka 20-49 au zaidi ya asilimia 40 waliolewa wakati wakiwa wadogo.
IMG_2233
Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA akizungumzia ufadhili wao wa dola 400,000 kwa ajili ya mradi wa elimu mbadala kwa wasichana walioacha shule kwa sababu za ujauzito wakati wa Mahafali ya Mradi huo mwishoni mwa wiki. Akina mama wadogo 149 walihitimu elimu hiyo kati ya 220 walioanza.Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito umefadhiliwai Ubalozi huo na kuratibiwa na UNESCO.
Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye kiwango cha juu cha ndoa a utotoni. Kwa wastani, mabinti wawili kati ya watano huolewa kabla hawajafikisha miaka 18.
Kwa hesabu za mwaka 2010 asilimia 37 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20-24 walikuwa wameolewa au kuwa na patna anayeishi naye kabla hawajatimiza miaka 18.
Hata hivyo takwimu zinaonesha kupungua kwa asilimia 10 tangu mwaka 2004 ikiwa ni sawa na asilimia 41.
Ingawa ndoa za utotoni ni kawaida nchini Tanzania mikoa yenye kasi kubwa ni Shinyanga (59%), ikifuatiwa na Tabora (58%), Mara (55%), Dodoma (51%), Lindi (48%), Mbeya (45%), Morogoro (42%), Singida (42%), Rukwa (40%), Ruvuma (39%), Mwanza (37%), Kagera (36%), Mtwara (35%), Manyara (34%), Pwani (33%), Tanga (29%), Arusha (27%), Kilimanjaro (27%), Kigoma (26%), Dar es Salaam (19%) na Iringa (8%).
Kama hatua hazitachukuliwa mabinti 1,382,000 ambaow atakuwa wamezaliwa kati ya mwaka 2005 hadi 2010 watakuwa wameshajiingiza katika mahusiano ya kuishi pamoja pamoja na kuelewa ifikapo mwaka 2030, hasa ikizingatiwa kuwa mwaka 2010 wanawake 764,000 wenye umri kati ya 20 hadi 24 walikuwa wameolewa au kuishi kinyumba kabla ya kutimiza miaka 18.
IMG_2201
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta akitoa salamu za UNESCO kwa niaba ya Mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_2117
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko (kulia) akiteta jambo na Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA wakati wa mahafali hayo.
IMG_2285
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko akitoa nasaha zake wakati wa mahafali hayo.
IMG_2130
Baadhi ya wahitimu wa kikundi cha Ujasiriamali cha Upendo Malunga wakitoa burudani ya shairi kwa mgeni rasmi na meza kuu.
IMG_1918
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (wa tatu kulia) na meza kuu wakikagua kazi mbalimbali za mikono zinazofanywa na wahitimu wa vituo mbalimbali ndani ya halmashauri ya Msalala wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_1922
Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa halmshauri ya Msalala,Vivian Masangya wakitazama ubora wa vitambaa vya meza vilivyotengenezwa na wahitimu hao.
IMG_1936
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko, Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila, Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA pamoja na Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta wakikagua kazi mbalimbali zilizofanywa na wahitimu hao kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_1977
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (kulia), akiwaunga mkono wakina mama hao kwa kununua shuka na foronya zilizotengenezwa na mmoja wa wahitimu hao (aliyebeba mtoto mchanga) wakati wa mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_1971
Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kushoto) akiwaunga mkono wahitimu hao kwa kununua Batiki wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_1975
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta akinunua batiki kutoka kwa mmoja wa wahitimu Hellena Masalu wa Kikundi cha Safina Kata ya Segese, mkoani Shinyanga wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_1964
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko akiwaunga mkono wahitimu hao wakati wa sherehe fupi ya Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_1984
Mmoja wa wakufunzi wa ujasiriamali halmashauri ya Msalala, Bi. Clemencia Mpuga Ngongo akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila, jinsi kifaa cha "Hydrometer" kinachotumika kupima wingi wa "Caustic" katika hatua za utengenezaji wa sabuni za kufulia za miche wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_2008
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila akikata miche ya vipande vya sabuni ta kufulia iliyotengenezwa na wahitimu hao.
IMG_2062
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila akishuhudia kwa vitendo utengenezaji wa sabuni za miche uliofanywa mbele yake kudhihirisha wahitimu wameiva kimafunzo.
IMG_2357
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (wa pili kulia) akimkabidhi cheti Mhitimu wa Lunguya, Shija Vicent wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_2350
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila akimpongeza Mhitimu wa kituo cha Lunguya, Fatuma Masaja mara baada ya kumtunuku cheti wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_2352
Mhitimu wa kituo cha Lunguya, Fatuma Masaja ambaye aliyepata ujauzito akiwa shuleni na uliompelekea kukatisha masomo yake na hatimaye mradi wa elimu mbadala kwa wasichana walioacha shule kwa sababu za ujauzito kumkomboa kwa kumpa mafunzo mbalimbali ikiwemo ujasiriamali wa kutengeneza batiki, sabuni, ushonaji n.k. akifurahia baada ya kutunukiwa cheti chake.
IMG_2139
Sehemu ya wakufunzi na wazazi waliohudhuria tukio hilo adhimu.
IMG_2393
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa vituo mbalimbali vya halmashauri ya Msalala vilivyohitimu mafunzo hayo.
IMG_2398
IMG_2405
IMG_2416
IMG_2388
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta akimpongeza kwa furaha mmoja wa wakufunzi walioshiriki kufanikisha mafunzo hayo Bi. Clemencia Mpuga Ngongo wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.

No comments:

Post a Comment