Pages

Thursday, September 3, 2015

HAYA NDIO MANENO YA ZITTO KABWE KUHUSU DK SLAA

Kiongozi Mkuu wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amejitokeza kumtetea Dk. Wilbroad Slaa dhidi ya majibu yanayotolewa na baadhi ya watu kufuatia hotuba yake aliyoitoa ikimtuhumu mgombea wa Chadema, Edward Lowassa kuwa fisadi asiyefaa kuchaguliwa kuwa rais.
Zitto ametumia akaunti yake ya Facebook kutoa mtazamo wake na uamuzi atakaochukua ingawa amekiri aliwahi kukwaruzana na Dk. Slaa alipokuwa Chadema na kupelekea kuondolewa katika chama hicho.
Hivi ndivyo alivyoandika:

 
Slaa hayupo kwenye karatasi ya kura. Naona watu wanahangaika na Slaa. Wengine tuliamua kukaa kimya kwani hekima inataka hivyo. Kwa kuwa watu wameamua kumtukana Dkt. Slaa ni lazima tutoke kulinda haki yake ya kusema yake. Tutatoka na tutaungana na Slaa kuwasema walio kwenye Ballot. Slaa hayupo kwenye Ballot. Mwacheni. Jadilini hoja zake sio kumjadili yeye. Eti hata watu wasio na rekodi yeyote ya kupambana na ufisadi nchi hii leo wanainua midomo yao kumsema Slaa. Mmeanza. Tutamsaidia Slaa, tutamaliza.
Sina mapenzi na Slaa. Alihusika kuniletea shida kubwa ya kisiasa nilipokuwa napigania MISINGI. Hata hivyo naipenda zaidi Tanzania kuliko tofauti zangu na Slaa. Ni lazima aheshimiwe na alindwe

No comments:

Post a Comment