Pages

Thursday, September 3, 2015

MISS TANZANIA HOI MAREKANI


Maskini! Miss Tanzania namba 2, 2005/06, Natalia Noel ambaye kwa hivi sasa anaishi katika Jimbo la Minnesota nchini Marekani, yupo taabani baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa mfumo wa damu (Lupus Nephritis) na kusababisha figo zake zote kushindwa kufanya kazi pamoja na moyo wake kuwa mkubwa hivyo kulala kitandani tu, wakati mwingine akisaidiwa na mashine ya kupumulia.
Akizungumza kwa tabu kwa njia ya mtandao kwa nia ya kupata mchango wa matibabu kwa ndugu na marafiki, Natalia alisema alianza kuumwa ugonjwa huo tangu mwaka 2008 na mara kwa mara alikuwa akionana na madaktari kwa ajili ya matibabu lakini ikashindikana.

 
Alisema kadiri siku zilivyozidi kusonga, ugonjwa huo ulisababisha kuharibu figo zake na moyo kuwa mkubwa hivyo kumpa tatizo la kupumua lililosababisha awe kwenye mashine ya kupumulia mara kwa mara.
“Maisha yamebadilika sana, zamani nilikuwa naweza kujifanyia kila kitu mwenyewe lakini si sasa, ugonjwa umenibadilisha sana, kwa sasa natakiwa nisafishwe damu yangu mara tatu kwa wiki (Dialysis) na zote hizo ni gharama kubwa sana kwangu, kwani tangu nianze kuumwa fedha zote zimeishia kwenye matibabu,” alisema Natalia kwa huzuni.
Mrembo huyo alikwenda nchini humo mara tu baada ya kumaliza mashindano hayo ya urembo na huko alikuwa akisoma na kuendelea na maisha yake.

No comments:

Post a Comment