Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 9, 2015

MUME AMCHARANGA MAPANGA MKEWE KISA WIVU WA MAPENZI

Ashura Ramadhani anayedaiwa kucharangwa mapanga na mumewe.
Na Haruni Sanchawa
WIVU! Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Abdallah, mkazi wa Gongo la Mboto, Ilala jijini Dar es Salaam, anadaiwa kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili mkewe Ashura Ramadhani kwa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili juzi kuwa Abdallah baada ya kufanya unyama huo, alikimbilia kusikojulikana na jeshi la polisi linamtafuta ili akabiliane na sheria.
Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto imethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo afisa mmoja alisema wawili hao walipeleka shauri lao hapo ambapo baada ya kusikilizwa, walikubaliana kila mmoja aishi kwenye chumba chake, uamuzi ambao hata hivyo, mwanamke aliupinga vikali.

Afisa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji, alisema mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa yao jambo ambalo mwanamke alilipinga. “Baada ya wawili hao kufika nyumbani, ugomvi ulianza tena ndipo mwanaume alimkata mkewe mapanga miguuni, kichwani na sehemu za siri,” alisema afisa huyo.

Ashura alipoulizwa na mwandishi wetu alikiri kutokea tukio hilo.
WIVU! Mtu mmoja aliyeju-likana kwa jina moja la Abdallah, mkazi wa Gongo la Mboto, Ilala jijini Dar es Salaam, anadaiwa kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili mkewe Ashura Ramadhani kwa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili juzi kuwa Abdallah baada ya kufanya unyama huo, alikimbilia kusikojulikana na jeshi la polisi linamtafuta ili akabiliane na sheria.
Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto imethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo afisa mmoja alisema wawili hao walipeleka shauri lao hapo ambapo baada ya kusikilizwa, walikubaliana kila mmoja aishi kwenye chumba chake, uamuzi ambao hata hivyo, mwanamke aliupinga vikali.
Afisa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji, alisema mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa yao jambo ambalo mwanamke alilipinga. “Baada ya wawili hao kufika nyumbani, ugomvi ulianza tena ndipo mwanaume alimkata mkewe mapanga miguuni, kichwani na sehemu za siri,” alisema afisa huyo.
Ashura alipoulizwa na mwandishi wetu alikiri kutokea tukio hilo.

No comments:

Post a Comment