Pages

Friday, September 4, 2015

SURA YA MTOTO WA DIAMONDITAONYESHWA KWA FEDHA SIKU YA AROBAINI YAKE



Diamond na Mtoto wake
MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ na mpenzi wake, Zarina Hassani ‘Zari’, wamekubaliana kutoonyesha sura ya mtoto wao wa kike, Tiffah hadi atakapofikia siku arobaini tangu kuzaliwa kwake.
Alisema makubaliano ya kuendelea kumficha mtoto huyo asionekane kwa jamii yametokana na makubaliano waliyonayo na makampuni mbalimbali yanayomdhamini.
Diamond alieleza hayo juzi katika kipindi kipya cha Uhondo kinachorushwa na Redio Efm chini ya uongozi wa Dinna Marios.
Alisema yeye na Zari walikuwa katika mazungumzo ya makubaliano na baadhi ya makampuni yanayotaka kuionyesha picha ya mtoto wao huyo kwa mara ya kwanza siku hiyo ya arobaini itakapofika.



“Hayo makampuni ndiyo yataionyesha picha ya mtoto wetu kwa mara ya kwanza siku hiyo ya arobaini itakapofika ndiyo maana tumekuwa tukijitahidi kuzuia watu wasipige picha na kuzisambaza mitandaoni hadi atakapotimiza siku hizo arobaini ili mchongo wetu usivuje,’’ alifafanua Diamond.

No comments:

Post a Comment