Pages

Friday, September 4, 2015

ZITTO KABWE AANDIKA UJUMBE MZITO KUHUSU DR SLAA


CHICKENS coming home to Roost
Mara baada ya JFK kupigwa risasi kule Dallas na kufariki dunia, wana habari walikwenda kwa Malcolm X kumuuliza maoni yake na jibu lake lilikuwa fupi tu "The Chickens came home to roost"
Kwa ufupi tu, X alieleza namna serikali ya Marekani ilivyoachia wazungu kunyanyasa, kuua na kutesa watu wa rangi nyingine kama Waafrika, bila ya kuwachukulia hatua yoyote. Hivyo, sasa weupe nao umefika wakati wapate madhila pia. Wamarekani walimlaani X kwa ajili ya kauli hiyo lakini ulikuwa ukweli.
Hiyo ndiyo hali inayomkuta Dk. Wilbrod Slaa hivi sasa. KUKU wake nao sasa wameanza kurudi bandani.



Kwa miaka takribani saba au nane sasa, Dk. Slaa alikuwa akishuhudia namna vijana wa chama chake walivyokuwa wakitukana watu mitandaoni, wakizushia watu mambo yasiyo ya kweli, wakidhalilisha na kuondoa utu wa watu.
Wakifukuzisha watu kazi kwa tuhuma za uongo, wakiharibu credibility ya watu walio credible na kumaliza maisha ya kisiasa ya watu ambao siasa zao zingekuwa na msaada mkubwa kwa taifa huko tuendako. Wote hawa waliharibiwa na Propaganda Machinery ya CHADEMA.
Nimeona watu wakilia machozi kwa kuumizwa kihisia na vijana wa CHADEMA, nimeshuhudia watu wakinyimwa kabsa haki ya kujieleza kwa sababu ya kuzidiwa na nguvu, shinikizo na kashfa za vijana wa chama hicho.
Kama isingekuwa tu uvumilivu wa aina yake, leo hii Zitto Kabwe angekuwa amekufa kabisa kisiasa au kimwili. Hii kazi ilifanyika vizuri na Dk. Slaa alikuwa miongoni mwa wafaidika wa siasa za namna hii.
Wakati huo, yeye alikuwa UNTOUCHABLE... Mguse Slaa uone kitakachokukuta.
Sasa leo, wafuasi wa kwenye mitandao na magazeti yaleyale yaliyokuwa yakimpamba na kumlinda kwa gharama yoyote, yameingia katika kazi ileile waliyozoea. Kwa bahati mbaya, mara hii Dk. Slaa ndiyo muathirika. Hiki anachokipata sasa, ndicho ambacho akina Zitto wamekuwa wakiishi nacho kwa miaka sasa.
Now, the Chickens are Coming Home to Roost, Dr. Slaa.

No comments:

Post a Comment