Kamanda wa
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP),Suleiman Kova akionyesha silaha kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani)walizozikamata kutoka kwa majambazi katika operesheni ya jeshi hilo
iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Na Chalila
Kibuda
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limevunja kambi inayodaiwa kuendesha
uhalifu wa kigaidi wa kuvamia vituo vya polisi na kunyanganya silaha kwa ajili
ya kuendeleza uhalifu na kuweza kukamata watuhumiwa saba.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema kundi
limenaswa kutokana na taarifa mbalimbali k mauaji ya kinyama na uporaji
silaha.
Amesema
kundi hilo linalodaiwa kuendeshwa na familia moja ya Ulatule limekuwa
likiendesha matukio mengi ya uhalifu ya kupora silaha katika vituo
vya polisi.
Wakati huo
Jeshi la Kanda Maalum ya Dar es Salaam,limewakamata watuhumiwa sita wa mauaji
wa Askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu Morogoro,Elibariki Pallangyo
lilolofanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kova amesema
katika tukio la kukamata watu hao kiongozi wao, Omary Salehe (Bonge Mzito)
alisema kuna silaha ikiwa ni njia ya kutaka kutoroka katika mikono ya polisi
ambapo polisi walitumia mafunzo yao vizuri na kufanikisha kumjeruhi na
alifariki wakati akipelekwa Hospitali.
Wengine ni
Said Mazinge (37) Mkazi wa Tegeta Kibaoni
Rashid
Watson (21)‘Dodo’Mkazi wa Vingunguti, Ramadhan Salum (38)’Nguzo
Mkazi wa Mbagala Kiburugwa Bakari Rashidi (38) ‘Malenda’
Mkazi wa Mbagala kizuiani Hamis Hamis (24) ‘Freemason Mkazi wa
Mbezi .
CHANZO: MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment