Richard Bukos aliyekuwa Manyara
BIBI mmoja anayeonekana kula chumvi nyingi, Jumapili iliyopita alijikuta akiangua kilio baada ya kuzuiwa kuzungumza na Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara, lakini alimsifia kiongozi huyo na kudai ndiye anayefaa kuiongoza Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete.
Katika tukio hilo, bibi huyo akiwa nyuma ya umati, alifanikiwa kujipenyeza katikati ya vijana na kumsogelea Magufuli aliyekuwa akimwaga sera na kuomba kura kwa ajili yake na wagombea wake wa ubunge na udiwani.
Akiwa chini ya jukwaa, bibi huyo alimsikiliza mgombea huyo akijinadi, ndipo alipoanza kumshangilia na kuwaomba askari waliokuwa karibu wamruhusu amng’ate sikio waziri huyo wa ujenzi, lakini alikataliwa na kutakiwa kukaa chini kwa utulivu.
Baada ya juhudi zake kushindikana, bibi huyo alianza kuangua kilio huku akisema alikuwa na ujumbe muhimu kwa mgombea huyo anayeamini ndiye rais ajaye na mkombozi wa kweli katika uongozi wa taifa hili.
“Huyu ndiye rais wetu anayetakiwa, naomba mniachie nikazungumze naye maneno machache nina jambo muhimu sana la kumwambia,” alisema bibi huyo akimuambia askari polisi aliyekuwa mbele yake ambaye hakumjibu lolote zaidi ya kumuangalia ‘kikauzu’.
Magufuli alikuwa akifanya kampeni hizo akitokea mkoani Singida ambapo alipita katika vijiji kadhaa na kurudi mkoani Dodoma katika wilaya mpya ya Chemba na baadaye alikwenda Kondoa hadi Babati mkoani Manyara ambako alifanya mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Akiwa kwenye kampeni hizo, mgombea huyo aliwaahidi wakazi hao kuwaondolea tatizo sugu la maji, kusambaza umeme vijijini, kujenga hospitali ya rufaa kila mkoa na kuanzisha viwanda katika vijiji kulingana na malighafi inayopatikana eneo husika.

No comments:
Post a Comment