Leo ni siku ya mwisho kwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es
salaam Suleiman Kova, kulitumika jeshi la Polisi nchini kwa kuwa muda wake wa
kulifanyia kazi jeshi hilo umeisha.
Kamanda Kova ametoa taarifa hiyo leo asubuhi alipokuwa
akizungumza kwenye cha asubuhi na ITV, na kusema kuwa mkataba wake na jeshi la
Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni.
"Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam
mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo
hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya
mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi,
mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu
wangu yupo atakuwa nanyi", alisema Kamanda Kova.
Kamanda Kova alikuwa Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es
salaam, na kwa mujibu wake amefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya
kiuhalifu, yaliyokuwa yanaitikisa nchi hususani matukio ya wizi na uvamizi wa
kwenye benki.
No comments:
Post a Comment