Ndege iliyokuwa safarini kutoka Mumbai kwenda London
ililazimika kukatiza safari na kurejea uwanja wa ndege baada ya panya kuonekana
ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo nambari AI 131 ilikuwa imefika Iran pale panya
alipoonekana na mmoja wa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo, ripoti zinasema.
Abiria waliendelea na safari yao kwa kutumia ndege nyingine.
Shirika la Air India limesema ndege hiyo itanyunyiziwa dawa
ya kuua wadudu na kwamba uchunguzi unafanywa kuhusu madai hayo ya kupatikana
kwa panya huyo.
Shirika hilo limesema wahandisi wa ndege wanaendelea na
uchunguzi “ingawa haijathibitishwa iwapo ni kweli kulikuwa na panya.”
Maafisa wa shirika hilo wamesisitiza kwamba uamuzi wa
kukatiza safari ulichukuliwa kwa maslahi ya usalama wa abiria.
Panya wanaweza kuwa hatari wakiwa ndani ya ndege kwani
wanaweza kutafuna nyaya.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment