Waziri wa Kilimo Mifugo na
Ushirika Mh. Mwigulu Nchemba akipokelewa katika ofisi ya Mkuu wa
Iringa na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mh. Amina Masenza na Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
Waziri wa kilimo Mh Mwigulu
Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na
kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa. Waziri wa kilimo Mh Mwigulu
Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na
kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa.
wakulima wamelalamika sana
uchelewashwaji wa pembejeo, bei duni ikiwemo madaraja mengi ya mfano
kuna madaraja zaidi 72 ya grade za tumbaku kitu ambacho wakulima
wamesema inawaumiza sana kwenye bei.
Pia wakulima wamelalamika
ubadhirifu wa chama cha mtandao (Union) kiitwacho ITCOJE. Katika ziara
hiyo Mh waziri aliambatana na Mrajisi wa vyama vya ushirika Dr.
Rutabanzibwa na Mkurugenzi wa bodi ya Tumbaku Bwana Mushi. Mh. waziri
ameagiza matatizo mengi yawe yametattuliwa kabla kikao cha bunge
hakijaanza.
Mh. Mwigulu aliwasili kwanza ofisi ya Mkuu wa mkoa na
kupokewa na Mkuu wa Mkoa Mh Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh
Richard Kasesela. Mh Masenza alimpa taarrifa fupi ya hali ya Kilimo
katika mkoa wa IRINGA.
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika mkutano
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika akisalimiana na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment