Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi hundi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa,ikishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(katikati)
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mgodi wa Bulyanhulu
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa akizungumza wakati wa ziara yake katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ambapo amesisitiza kuwa kodi ya ushuru wa huduma iliyotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu itumike vizuri kujenga miundombinu ambayo wananchi wataiona kwa macho
Afisa Maendeleo na Mahusiano wa mgodi wa Bulyahulu ,Sara Teri akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa,kushoto kwake ni Mshauri wa Mahusiano ya Kampuni ya Acacia na Serikali , Alex Lugendo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa (Kushoto) akielekea katika eneo la mgodi wa chini ya ardhi Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya kahama Vita Kawawa na ujumbe wake pamoja na mshauri wa mahusiano ya kampuni na serikali wa Acacia aliyesimama katikati mwenye shati ya bluu Alex Lugendo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa chini ya archi kilomita moja kutoka uso wa dunia akiwapongeza wafanyakazi wazawa katika mgodi wa Bulyanhulu kwa kufanya kazi ambazo zamani watanzania walikuwa hawawezi, kazi ya kufanya kazi kwa mitambo ya kisasa ya inayojulikana kama Jumbo na mashine zingine za teknolojia ya kisasa zinazotumika katika kuchimba dhahabu kwenye mgodi mkubwa wa dhahabu nchini Bulyanhulu.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa anatoka kwenye lifti kutokea chini ya ardhi baada ya kutembelea mgodi wa dhahabu chini ya ardhi.
Kaimu Meneja wa Uchimbaji katika Mgodi wa Bulyanhulu Salvatory Tesha
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Bw.Graham Crew akifafanua jambo kwa mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa.
Meneja wa Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila akimuonyesha ramani ya uchimbaji mkuu wa Wilaya ya Kahama na ujumbe wake
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuwa fedha zitumike vizuri katika miradi inayoonekana.
“sitaki masuala ya kusema unajua pesa tuliitumia katika kuweka kifusi barabarani na sasa mvua imekiosha, hapana, hilo litakuwa ni jipu linatakiwa kutumbuliwa, fedha hizi zitumike kujenga miradi inayoonekana kama vila vyumba vya madarasa, zahanati nakadhalika.”
No comments:
Post a Comment