Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Sarah Martin aliwasomea
mashtaka washtakiwa hao, Mweka Hazina, Hafidhi Mgagi, Mhasibu Gershom Bwire na
Sanga.
Sarah alidai kuwa washtakiwa hao walimdanganya mwajiri wao
na kujipatia fedha kwa kutumia nyaraka za kughushi na kuisababishia Serikali
hasara ya Sh4 milioni.
Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa Sanga na Mgagi kati ya
Novemba 23 hadi 28, 2012 waliidhinisha malipo ya Sh4 milioni kwa Gershom Bwire
kutengeneza vitabu 150 vya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa
(LAAC).
Alidai kuwa katika shtaka la pili mshtakiwa wa tatu, Bwire
Novemba 23 na 28, 2012 alijipatia fedha isivyo halali, mali ya mwajiri.
Mwendesha mashtaka alidai kuwa washtakiwa hao wameitia
hasara halmashauri kwa kujipatia Sh4 milioni.
Washtakiwa walikana
mashtaka na kuachiwa kwa dhamana. Hakimu wa mahakama hiyo, Rashid Chaungu
aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 17.
No comments:
Post a Comment