Balozi wa Uswisi nchini, Florence Tinguely Mattli akitoa neno la ufunguzi katika mdahalo huru kuhusu ajira kwa vijana
Wachangia mada katika mdaharo huru kuhusu ajira kwa vijanaBaadhi ya washiriki waliohudhuria mdahalo huo
Katika kuadhimisha miaka 50 ya mahusiano na ushirikiano baina ya Uswisi na Tanzania, ubalozi wa Uswisi nchini umefanya mdahalo wa wazi kuhusu ajira kwa vijana ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kubadilishana mawazo jinsi wao wanavyofanya ili kupambana na tatizo la ajira.
Mdahalo
huo ambao ulifanyika katika hoteli ya Coral Beach, jijini Dar es Salaam
ulijadili mambo mbalimbali ambayo yanasababisha kuwepo kwa ajira chache
lakini pia uwezo wa vijana wa kuingia katika soko la ushindani la
ajira.
Aidha
mdahalo huo uliweza kujadili kuhusu changamoto iliyopo ya ajira kwa
vijana na kuependekeza njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili
kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaonekana kukua kwa jinsi siku
zinavyokwenda.
Wakizungumza
na Mo Dewji Blog baada ya kumalizika kwa mdahalo huo wadau mbalimbali
ambalo walihudhuria walisema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana
linaanzia katika aina ya sera ambazo serikali inazitumia katika sekta ya
elimu kushindwa kufanya kazi katika soko la ajira la sasa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema kuwa ili serikali kupunguza
tatizo la ajira kwa vijana inatakiwa kuhakikisha inaimarisha uchumi wa
nchi lakini ambao unatoa nafasi za ajira zaidi.
Alisema
mbali na kuimarisha uchumi pia inatakiwa kuwatengenezea wananchi wake
mazingira mazuri ambayo yatawashawishi kujiajiri bila kutegemea ajira ya
serikali au makampuni binafsi ambayo kwa sasa ndiyo yanaonekana kutoa
nafasi nyingi za ajira.
“Vijana
wengi kwa sasa wakimaliza vyuo wanajiajiri na hata kama wanauza
barabarani korosho huko nako ni kujiajiri … serikali inatakiwa
kuimarisha uchumi wa nchi na sio kukuza tu lakini ukue na utoe fursa za
ajira kwa wazawa,” alisema Eyakuze.
Aidha
aliwataka vijana kuacha tabia ya kutegemea ajira za serikali na sekta
binafsi kwani ushindani katika soko la ajira ni mkubwa na kama wanakuwa
hawajajiandaa kwa kiasi kinachohitajika sasa katika soko la ajira basi
inaweza kuwa ngumu kwao kupata nafasi.
Nae
Amabalis Batamula kutoka Femina alisema sera ambazo zinatumika nchini
hazitekelezwi kama zinavyopangwa na serikali na pia hazina faida kwa
soko la ajira la sasa kutokana na kubadilika kwa jinsi miaka inavyozidi
kwenda.
Alisema
ni jambo la ajabu baadhi ya sera za elimu ni kuendelea kutumika hadi
sasa licha ya soko la ajira kubadilika na hivyo kuhitaji sera mpya
ambazo zinakwenda na wakati lakini pia kuwashauri vijana wanaohitimu
kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake wawe wakijiajiri ili kuepuka
tatizo la ukosefu wa ajira.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), inaonyesha
kuwa zaidi ya vijana 800,000 humaliza chuo kila mwaka na wanaokadiriwa
kupata ajira rasmi ni 40,000 pekee hivyo kuonyesha ni jinsi gani kuna
upungufu mkubwa wa ajira nchini.
Mmoja wa washambuzi wa mada akielezea jambo katika mdahalo huru kuhusu ajira kwa vijana Washiriki wa mdahalo wakiwa katika makundi kujadili mada zilizotolewa
Unaweza kusikiliza hapa baadhi ya washiriki waliozungumza na Mo Dewji Blog
No comments:
Post a Comment