Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), alipokutana nao kabla ya kuongea na Wafanyakazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye koti la kaki), akisisitiza jambo kwa Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),alipokutana nao jijini Dar es Salaam.
Rubani Lilla Borri wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Wafanyakazi wa Shirika hilo na Waziri Prof. Mbarawa, uliofanyika katika ofisi za Shirika hilo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiagana na
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), mara baada ya kuongea nao
Ofisini Hapo.
SERIKALI
imezungumzia umuhimu wa kulifufua upya Shirika la Ndege nchini Air Tanzania
(ATC) kwa kulinunulia ndege mpya na kulipa mtaji ili lifanye kazi kibiashara na
kutengeneza faida kama ilivyokusudiwa awali.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Pichani)ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na menejimenti na wafanyakazi wa Shirika hilo alipolitembelea
jijini Dar es Salaam leo.
“Tutawekeza
kwenye Air Tanzania ili kuongeza fursa za kiuchumi na kuvutia wasafiri wengi
kufika nchini moja kwa moja na kuvutia sekta ya utalii”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri
Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Shirika hilo ambao sio waadilifu na
wavivu kuondoka mara moja ili kupisha wafanyakazi wabunifu na wenye mawazo ya
kibiashara kuendesha shirika hilo kwa faida.
“Tunataka
watu watakaolitoa shirika hili kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kuliwezesha
kiuchumi na kujitegemea ili kushindana na mashirika mengine ya ndege katika biashara“,
amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli
yuko tayari kununua ndege mpya ili kulifufua shirika hili hivyo amewataka
wafanyakazi hao kuwa na mtazamo chanya wa kufanya biashara ili kuiletea taifa
tija.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATC Bw. Johnson Mfinanga amemwambia Waziri
Prof. Mbarawa kuwa kwa sasa shirika hilo lipo katika hali mbaya kiuchumi na
hivyo kuhitaji nguvu ya Serikali kulikwamua ili litoe huduma inayoshahili.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali itaangalia upya taratibu za
ajira katika shirika hilo na watakaobainika kuajiriwa kinyume cha taratibu
watafukuzwa kazi mara moja.
“Tutanataka
watu waadilifu, wabunifu na wenye sifa stahiki ili wafanye kazi kwa maslahi ya
shirika na taifa kwa ujumla”, amefafanua Waziri Mbarawa.
Shirika
la Ndege nchini ATC toka mwaka 2009 limekuwa likijiendesha kwa hasara na
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kulifufua shirika hilo ili lifanye kazi
kwa faida na kuboresha usafiri wa anga ndani na nje ya nchi na hivyo kuvutia
wasafiri wengi kuja nchini moja kwa moja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano.chanzo Issa MIchuzi
No comments:
Post a Comment