Pages

Thursday, March 17, 2016

WAZIRI MWAKYEMBE ATOA RAI KWA TAASISI MBALIMBALI NA WADAU KUIPITIA RIPOTI YA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA ILI KUBORESHA CHAGUZI ZINAZOKUJA


Mgeni rasmi,Waziri wa sheria na Katiba Dkt Harrison Mwakyembe akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na Ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita,aliyoipokea kutoka kwa Waandaaji  CEMOT (umoja wa taasisi za waangalizi wa ndani wa uchaguzi inayohusisha Kamati ya Uangalizi wa Uchaguzi (Temco) na Muungano wa taasisi zisizo za kiraia za kusimamia uchaguzi (Tacceo) ),kwenye semina iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Hyatt Hotel jijini Dar na kuwakutanisha Wadau mbalimbali wakiwemo Tume ya Uchaguzi (NEC),Polisi,PCCB pamoja na Nchi Wahisani .Pichani kushoto ni Mjumbe wa kamati ya CEMOT Bwa.Ezekiel Massanja

Katika mahojiano mafupi na Waandishi wa habari mara baada ya kuipokea ripoti hiyo,Dkt Mwakyembe alisema kuwa Ripoti hiyo iliangalia mapungufu yaliyokuwepo na namna ya kuyaboresha,Dkt Mwakyembe ametoa rai kwa Serikali,taasisi mbalimbali na wadau wengine waweze kuipitia ripoti hiyo na kujadiliana ili kuboresha chaguzi nyingine zinazokuja.
 Wa pili kulia ni Mgeni rasmi,Waziri wa sheria na Katiba Dkt Harisson Mwakyembe akiandika jambo wakati ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita,aliyoipokea kutoka kwa Waandaaji  CEMOT  ikisomwa.

 
 Mkuu wa Waandaaji wa Ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita (CEMOT),Dkt.Alexander Makulilo akisoma ripoti hiyo mbele ya Wadau na walioshiriki kuiandaa ripoti hiyo.
  Baadhi ya Wadau walioshiriki kundaa Ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita,wakifuatilia kwa makini wakati ripoti hiyo ikisomwa. 

No comments:

Post a Comment