gari ikiwa imetumbukia mtaroni baada ya kupata ajali wakati mabrazameni hao wakijaribu kukimbia baada ya kupasua kioo cha noah na kuiba simu na vitu vingine.
Hawa ndio mabrazameni wenyewe hebu wacheki walivyo watanashati lakini kumbe ni wezi.Hivi karibuni kumeibuka wizi wa kupasua vioo vidogo vya magari kwa kutumia dawa maalumu then wanaiba vitu kama simu,laptop na vitu vingine vidogo.Na wakati wanaiba wanakua na gari nyingine wakimaliza hukimbia kwa kutumia gari,Habari kamili soma chini.
Hapa mabrazameni hawa wakiwa hoi kwa kipigo heavy na kuokolewa na polisi vinginevyo walikuwa wanachomwa moto na wanainchi wenye hasira.
HABARI KAMILI
Vijana wawili ‘mabrazameni’ waliofahamika kwa majina ya
Rashid Kasim ‘Mwarabu’ (27) na Kassim Said (25), hivi karibuni walikumbwa na
msala baada ya kuchezea kichapo wakidaiwa kufanya tukio la wizi maeneo ya Mbezi
jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea Septemba 28, mwaka huu ambapo inadaiwa jamaa hao walimwibia fedha pamoja na simu mtu mmoja (jina linahifadhiwa kwa sasa) vilivyokuwa ndani ya gari lake.

Akizungumza hivi
karibuni, shuhuda mmoja wa tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema
kuwa jamaa aliyeibiwa alifika maeneo ya Bahari Beach, Mbezi kwa lengo la
kumsalimia rafiki yake na ndipo alipokutwa na balaa hilo.
Yule jamaa alifika pale kumsalimia rafiki yake, akapaki gari
lake aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili T 940 BCL nje na kuingia
ndani. Akiwa ndani, wakatokea jamaa wawili, wakavunja kioo kisha kuiba simu na
pesa zilizokuwa mle ndani.
“Watu wakaanza kupiga kelele za wizi, mwenye mali akatoka, jamaa wakatoka nduki wakiwa na gari lao aina ya Toyota Corona lenye namba za usajili T 243 AUS. Wakaanza kukimbizwa, gari lao halikufika mbali, likazingirwa na watu wakaanza kuwashushia kipigo,” alisema mtoa habari huyo.
Akaongeza kuwa, kutokana na hasira walizokuwa nazo watu hao, walifikia hatua ya kutaka kuwachoma moto lakini jitihada za kuwaita polisi zilifanyika ambapo vijana hao waliokolewa.
“Kama siyo polisi kufika, tungekuwa tunaongelea mambo mengine, gari lao lilishambuliwa kwa mawe likawa nyang’anyang’a, watu wakataka kuwachoma moto lakini bahati ilikuwa yao kwani polisi walizuia zoezi hilo,” alisema sosi huyo.
Ikaelezwa kuwa baada ya polisi kufika waliwachukua watuhumiwa hao pamoja na jamaa aliyeibiwa na kwenda nao kituoni ambapo jalada la kesi lenye namba KW/RB/7885/2011 WIZI TOKA GARINI lilifunguliwa.
Mpaka tunakwenda mtamboni, uchunguzi juu ya tukio hilo ulikuwa ukiendelea ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

No comments:
Post a Comment