skip to main |
skip to sidebar
ruvu wapiga mtibwa sugar
JKT
Ruvu imeichapa Mtibwa Sugar mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu ya
Tanzania iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es
Salaam.Kwa ushindi huo klabu ya JKT Ruvu imefikisha pointi 15 kama
ilizonazo klabu za Mtibwa Sugar na Azam.
Mtibwa
ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya tisa lililofungwa
na Vicent Barnabas aliyeunganisha krosi ya Issa Rashid.JKT Ruvu
walisawazisha bao hilo katika dakika yabaada ya Mtibwa kujifunga
wenyewe wakizembea kuondoa mpira wa kona.
JKT
Ruvu pia waliongeza bao la pili kupitia kwa Rajab Chau aliyepokea mpira
wa faulo ndogo uliopigwa na Emmanuel Linjechele.Timu hizo mpaka
zinaenda mapumziko JKT Ruvu ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1, lakini
katika kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa kushambuliana.
Kipindi
cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji, lakini mabadilko
hayo yalionekana kuwasaidia zaidi JKT Ruvu kwa sababu walipata penati
katika dakika ya 85 ambayo ilifungwa na Stanley Nkomola na kuandika bao
la tatu.
Penati
hiyo ilipatikana baada ya Hussein Bunu kudondoshwa na Salvatory Ntebe
katika eneo la hatari na mwamuzi Amon Paul wa Mara aliamuru ipigwe
penati.Slavatory Ntebe aliipatia Mtibwa bao la pili katika dakika ya 89
baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa JKT, Hamis Seif.
Ligi
Kuu itaendelea tena Oktoba 14 kwa Yanga kucheza na Kagera Sugar, halafu
Oktoba 15 JKT Ruvu itacheza na Azam, pia Oktoba 16 Simba itacheza na
African Lyon.
No comments:
Post a Comment