Naibu
waziri wa Uchukuzi, Enjinia Dakitari Athuman Mfutakamba (Mbunge)
akimkabidhi bendera Vodacom Miss Tanzaia 2011, Salha Israel tayari
kuiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo wa Dunia (Miss World
2011) yaliyopangwa kufanyika London, Uingereza Novemba 6.
Mbali
ya kukabidhi bendera, Naibu Waziri pia alimchangia salha Dola 1000 kwa
ajili ya safari hiyo huku wafanyakazi wa wizara yake wakitoa Shs
Milioni 3.4.
Pia
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kilikabidhi Dola 2000 mrembo huyo
kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, Nakuala Senzia.
Senzia
pia alimkabidhi Salha kifurushi kinachoelezea vivutio vya utalii na
uwekezaji vya Tanzania ambavyo Salha atavitumia wakati wa kuinadi nchi
akiwa kambini na mashindano hayo. Picha na Maelezo kwa Hisani ya
kitengo cha Habari cha Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment