HAROUB CANAVARO AONDOLEWA TAIFA STARS

Beki
wa kati wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Nadir Haroub
ameondolewa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini
N’Djamena.
Haroub ameondolewa baada ya kuumia kifundo cha mguu wa kulia (right ankle) akiwa mazoezini jana asubuhi (Novemba 5 mwaka huu).
Kwa
mujibu wa daktari wa Stars, Dk. Juma Mwankemwa, mchezaji huyo
hakuvunjika isipokuwa amepata mshtuko mkubwa wa kifundo hicho ambapo
itamchukua wiki mbili kupona sawa sawa.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amesema kutokana na hali hiyo Haroub
hatakuwemo kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mechi hiyo na ile ya
marudiano ambayo itachezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Poulsen
amesema kwa muda uliobaki hataita mchezaji mwingine kwa ajili ya
kuziba pengo la Haroub, hivyo kwa sasa atabaki na kikosi cha wachezaji
21 alionao kambini hoteli ya New Africa.
No comments:
Post a Comment