Pages

Monday, November 7, 2011

HAROUB CANAVARO AONDOLEWA TAIFA STARS

HAROUB CANAVARO AONDOLEWA TAIFA STARS

Beki wa kati wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Nadir Haroub ameondolewa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.
Haroub ameondolewa baada ya kuumia kifundo cha mguu wa kulia (right ankle) akiwa mazoezini jana asubuhi (Novemba 5 mwaka huu).
Kwa mujibu wa daktari wa Stars, Dk. Juma Mwankemwa, mchezaji huyo hakuvunjika isipokuwa amepata mshtuko mkubwa wa kifundo hicho ambapo itamchukua wiki mbili kupona sawa sawa.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amesema kutokana na hali hiyo Haroub hatakuwemo kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mechi hiyo na ile ya marudiano ambayo itachezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Poulsen amesema kwa muda uliobaki hataita mchezaji mwingine kwa ajili ya kuziba pengo la Haroub, hivyo kwa sasa atabaki na kikosi cha wachezaji 21 alionao kambini hoteli ya New Africa.

No comments:

Post a Comment