Pages

Wednesday, November 9, 2011

JOE BOSINGWA: nahisi kudhalilishwa.

JOE BOSINGWA: nahisi kudhalilishwa.

Joe Bosingwa wa Chelsea mwenye jezi ya bluu kwenye mechi na Wolvermpton
Mlinzi wa Chelsea Jose Bosingwa ameweka wazi kuwa hatoichezea tena timu yake ya taifa ya Ureno mpaka kocha wa sasa wa timu hiyo Paulo Bento atakapoondoka kwenye nafasi hiyo.
Bosingwa aliachwa katika kikosi kitakachocheza play off ya Euro dhidi ya Bosnia na Herzegovina, huku Bento akiwa na mashaka huu ya mentality na tabia ya Bosingwa.
Akizungumza leo Bosingwa amesea “Sijui nini anachoongea kuhusu maoni yake juu mentality na altitude yangu, Nahisi kudhalilishwa na kutoheshimiwa kutokana na maneno yake, sasa Sitovaa tena jezi ya Portugal kama huyu kocha akiendelea kuwa kwenye benchi”
“Jamii nzima inatambua juu ya tabia ya kocha huyu, haelewani na wachezaji na anagombana nao kila mara, hana uwezo wa kiakili wala kihisia kuongoza kundi la wanaume na hafai kabisa kuiongoza timu ya taifa.”
Bosingwa anakuwa mchezaji wa pili wa Ureno kuamua kustaafu kuichezea Ureno, baada ya beki wa Real Madrid Ricardo Carvalho kujiondoa katika timu hiyo baada ya kugombana na kocha huyo

No comments:

Post a Comment