Wananchi
wakitazama Stationery ya Nyigi iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso
ambayo imevunjwa na wezi
Mmiliki
wa duka la Ferick Urembo akiangua kilio kwa uchungu baada ya
kukuta duka lake limevunjwa na kuibwa mali mbali mbali asubuhi hii.
NA
FRANCIS GODWIN
Wakati maandalizi ya sikuu kuu za
Krismas na mwaka mpya yakianza taratibu ,watu wanaosadikika kuwa ni
wezi nao wameanza kufanya maandalizi ya funga mwaka baada ya
usiku wa leo kuvunja maduka mawili eneo la Eso katika Manispaa ya
Iringa na kuiba mali mbali mbali.
Maduka ambayo yamevunja usiku wa leo
ni pamoja na duka la Ferick Urembo lililopo eneo la Natioanl katika
majengo ya Bakwata , na Nyigu Stationery iliyopo eneo la jengo la
Masiti Eso.
Baadhi ya wamiliki wa maduka hayo
wamesema kuwa maeneo yao yamekuwa yakilindwa na makampuni ya
ulinzi na hadi sasa eneo la tukio walinzi wa wamu hawapo.
Katika duka la Ferick Urembo watu
hao wanaosadika kuwa ni wezi wamechukua mali mbali mbali ukiwemo
urembo vyote vikikisiwa kufikia kiasi cha TS.milioni zaidi ya 2 huku
katika Stationery ya Nyigu kompyuta na mali mbali mbali zimechukuliwa
na ambavyo vyote thamani yake bado kufahamika .
Mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com umefika eneo la tukio na kushudia
vilio vikiwa vimetawala kwa wamiliki wa maduka hayo tukio ambalo
bado limekusanya umati mkubwa wa watu
No comments:
Post a Comment