Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 24, 2011

Ajali Mbaya Yaua Wawili Babati


Walioteketea kwa moto inadhaniwa kuwa ni dereva na tandiboy waFuso ambao walibanwa katika gari hilo baada ya kukatika cabin.
Fuso ilivyoteketea kabisa na moto.
Watu zaidi ya wawili wanahofiwa kufa katika ajali ya gari iliyotokea usiku majira ya saa 6 katika eneo la kijiji cha Mdori Wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo watu wawili walionekana miili yao ikiwa imeungua na moto. Ajali hiyo ililihusisha roli la mizigo lililokuwa limetokea Arusha na Fuso lililokuwa limetokea Singida.
Mafuta ya kupikia ya alizeti yalitapakaa katika eneo hilo.
Wanawake wa Kijiji cha Kadori wakichota mafuta yaliyomwagika katika ajali hiyo.Lakini je mafuta haya yaliyomwagika chini ni safi na salama kwa afya

No comments:

Post a Comment