Aliyekuwa mkuu wa ujasusi katika utawala wa Kanali Gaddafi Abdullah al-Sanussi amekamatwa, serikali ya mpito ya Libya imesema.
Alikamatwa na wapiganaji kusini mwa nchi.
Bwana Sanussi,alikuwa mmoja wa viongozi wakuu katika serikali ya Gaddafi ambaye alikuwa hajulikani alipo.
Mwanawe
Gaddafi Saif al-Islam alikamatwa siku ya Jumamosi. Wote,yeye na Bwana
Sanussi wanatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita na mahakama ya kimataifa ya
jinai.
Bwana
Sanussi, ambaye ni shemeji yake Kanali Gaddafi, inasemekana alikamatwa
nyumbani kwa dada yake katika mji wa Sabha ulioko kusini mwa nchi siku
ya Jumapili.
Alifahamika kama mtu wa karibu wa marehemu Gaddafi - na mmoja wa watu waliogopewa sana katika utawala huo.
Bwana
Sanussi, 62, anatuhumiwa na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa
kuhusika na ukatili wakati wa kuzima maandamano dhidi ya utawala wa
Gaddafi mapema mwaka huu.
Pia
ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu, ikiwemo kuhusishwa kwa
mauaji ya wafungwa zaidi ya 1,000 katika gereza la Abu Salim mjini
Tripoli mwaka 1996.
No comments:
Post a Comment