Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, November 21, 2011

WAZIRI DK. MARY NAGU AONGEA NA WANA AZAKI UBUNGO PLAZA JIJINI DAR ES SALAAM


Mheshimiwa Mary Nagu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji akiongea na washiriki wa tamasha la AZAKI wakati akiongea nao wakati kifungua tamashya hilo lililoanza leo kwenye Ubungo Plaza kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es salaam, tamasha hilo ambalo linaambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za wana AZAKI yatafanyika kwa siku tatu mfurulizo.
Mkurugenzi wa Asasi za Kiraia AZAKI Bw. John Ulanga akizungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo kabla ya Waziri Dk. Mary Nagu kufungua tamasha hilo asubuhi hii katika hoteli ya Bleu Pearl.
Mmojawa wa washiriki ambaye ni mlemavu wa ngozi akiandika mambo muhimu ya yaliyokuwa yakizungumzwa na Waziri Dk. Mary Nagu wakati akifungua mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa Tamasha hilo wakimkaribisha Waziri Dk. Mary Nagu wakati alipokuwa akiiingia katika ukumbi wa mkutano tayari kwa kuzindua tamasha hilo asubuhi hii

No comments:

Post a Comment