RIO ASHANGAZWA NA KAULI YA BLATTER KUHUSU UBAGUZI.
BEKI
wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United Rio
Ferdinand amesema amshangazwa na madai ya Rais wa Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA Sepp Blatter akidai kuwa hakuna ubaguzi katika mchezo wa
mpira uwanjani. Blatter alijichanganya katika kauli yake akzungumzia
suala la ubaguzi uwanjani kuwa linaweza kutatuliwa kwa wachezaji kupeana
mikono baada ya mchezo ingawa baadae alidai kuwa ameeleweka
vibaya. Katika mtandao wa kijamii wa Twitter Ferdinand aliandika ujumbe
wa kuonyesha kushangazwa na kauli hiyo kwa kusema kuwa anaweza kuwa
amekosea kusoma matamshi ya Blatter aliyotoa na kama hajakosea kosea
kusoma basi ameshangazwa na kauli ya kiongozi huyo. Ferdinand baadae
alimtumia ujumbe kwa Blatter. Katika ujumbe huo aliosema kuwa matamshi
yake kuhusiana na ubaguzi yanashangaza na kwa kweli yanachekesha na
iwapo mashabiki watapaza sauti zao kwa maneno ya kibaguzi jee kushikana
mikono hapo ni sawa? Matamshi ya Blatter yamekuja wakati nahodha wa
Chelsea John Terry akichunguzwa na polisi pamoja na Chama cha Soka cha
Uingereza-FA juu ya tuhuma za kumtamkia maneno ya kibaguzi mlinzi wa QPR
Anton Ferdinand, ambaye ni mdogo wake Rio.
No comments:
Post a Comment