Pages

Saturday, November 5, 2011

RIPOTI YA CAG KUANIKA UBADHIRIFU, WANANCHI SENGEREMA WAITAKA KAMATI YA MREMA


Na Mashaka Baltazar,MWANZA
WANANCHI WA Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, wameitaka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa, kufika wilayani humo ili kujionea uozO na ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Sakata hilo limeibuka hivi karibuni katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, kufuatia ripoti ya ukaguzi maalumu, uliofanywa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Fedha za Serikali (CAG) Ludovick L. Utoh, baada ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Matthew Lubongeja kuwataka madiwazni wasijadili ripoti hiyo akidai ilikuwa ya siri.
Madudu hayo ya ubadhirifu wa fedha za umma yameibua mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, kufuatia ofisi ya CAG, kuanika katika ripoti ya ukaguzi wake ubadhirifu mkubwa wa fedha za miradi ya maendeleo.
Kutokana na ubadhirifu huo CAG amependekeza uongozi wa halmashauri hiyo, uwachukulie hatua za kinidhamu na kuwasimamisha kazi watendaji wake tisa kwa madai ya kukiuka sheria, taratibu na kanuni za utendaji kazi.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa watendaji wa halmashauri hiyo hawafuati sheria,taratibu na kanuni katika utendaji wao kazi kuhusiana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri, ambapo pia ilibaini kuwa fedha shilingi bilioni 1.5 zilitengwa kwa ajili ya idara ya kilimo hazikutumika bila sababu katika kipindi cha miaka miwili.
Madiwani hao walipinga kutojadiliwa kwa ripoti hiyo ikiwa ni pamoja na kuukataa ushawishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo Elinansi Pallangyo kutotaka ijadiliw, waaakidai kuwa kikao hicho ndicho chenye maamuzi ya mwisho
Kwa mujibu wa chanzo chetu madiwani hao walichachamaa na kutaka ripoti hiyo iletwe na kujadiliwa kisha kuchukua hatua kulingana na mapendekezo ya CAG, ambapo Mwenyekiti baada ya kuzidiwa nguvu alimwagiza Mkurugenzi wa halmashauri Eric Mussika kuileta na ikapitiwa kifungu kwa kifungu.
Madiwani baada ya kupitia ripoti hiyo walibaini kutokamilika kwa miradi mingi ya maendeleo, wakati fedha zimetolewa kwa ajili ya miradi ya maji,barabara na ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu, huku miradi mingine fedha zikiwa zimehamishwa bila idhini ya vikao kutoka akaunti moja kwenda nyingine.
Katika ripoti hiyo ya ukaguzi huo CAG (nakala tunayo) ilibaini kuwapo kwa ucheleweshaji wa ujenzi wa majengo nabaadhi yamejengwa chini ya kiwango hivyo kutolingana kwa thamani ya fedha zilizolipwa kwa wakandarasi.
Mmmoja wa Madiwani wa halmashauri hiyo alisema kuwa waqtendaji hao hawafuati sheria za manunui na hakuna uwazi wan a musada wa kutosha katika utangazaji wa zabuni mbalimbali , kweamba halmashauri haina daftari la kumbukumbu ya miradi husika kwa mujibu wa agizo Na.6(e) na 50 ya kanuni ya fedha za Serikali za Mitaa,ya mwaka 1997.
“Kwa ujumla CAG amebaini ubadhirifu katika miradi ya ujenzi wa majengo,barabara na maji.Watendaji wa halmashauri wanakiuka sheria za manunuzi ya umma kwa kutozuingatia kifungu cha 37 (4) ya sheria ya manunuiz ya umma , kumesababisha uteuzi wa wajumbe wa timu ya tathmini wasio na ujuzi wa kai yauthamini” alisema mmoja wa madiwani kwa sharti la kutojwa jina
Alisema ripoti ya mkaguzi huyo wa hesabu za serikali ilileza kuwa halmashauri hiyo haina mchanganuo wa kazi unaojumuisha kodi la ongezeko la thamani na inamtaja Mhandisi wa Maji Elikali Edward kuwa, uzembe wa kutoandaa makisio ya ufanyaji kazi kabla ya mradi kuanza na ni moja ya mapungufu yanyoisababishia hasara halmashauri hiyo.
Wengine waliotajwa katika ripoti hiyo maalumu ni pamoja na Afisa Mipango wa Wilaya hiyo,Kaimu Mweka hazina,Mwenyekiti wa Bodi ya zabuni, Afisa Ugavi wa Wilaya,Mhandisi wa Ujenzi, Mwanasheria wa Halmashauri, Meneja wa Mamlaka ya maji safi na majitaka na Mhasibu wa Mamlaka ya maji safi na majitaka.
Aidha Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lubongeja alitaka hoja hiyo ya kusimamishwa kwa watendaji hao iahirishwe hadi Novemba 6 mwaka huu ili Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , Ndikilo aweze kuhudhuria.
Mmoja wa madiwani wa halmahauri hiyo, Hamis Tabasamu alipinga hoja hiyo akidai kuwa ni kupoteza fedha za walipa kodi kwa vile kikao kimoja hugharimu shilingi milioni 16 za kulia posho wajumbe 46 ambapo kila mmoja hulipwa shilingi 175,000 hali iliyosababisha atolewe nje ya kikao na mwenyekiti, baada ya kusisitiza watumishi waliotajwa katika ripoti hiyo ya CAG wasimamishwe kisha mashitaka yao yafuate kama ilivyobainisha taarifa hiyo ya ukaguzi maalum.
Wananchi wa wilaya hiyo wamedai kuwa kama watumishi hao hawaatchukuliwa hatua basi hawana imani na uongozi wa halmashauri hiyo chini mwenyekiti na mkurugeni wake na kupendekeza kamati ya bunge ya seriali za mitaa kufanya uchunguzi wa ubadhirifu huo .
Endapo hilo halifanyika basi wananchi hao wako tayari kuifikisha halmashauri yao mahakamani ikiwa ni pamoja na mwenyekiti kwa madai kuwa alishiriki kusaini mikataba mibovu isiyo na tija.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG ambayo nakala yake imepelekwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, inawataka makandarasi waliolipwa bila kufuata taratibu kurejesha fedha hizo halmashauri, wengi wakiwa ni wale waliopewa zabuni za miradi ya majengo, maji na barabara.

No comments:

Post a Comment