Mzee
Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), akiwa hoi jana
siku ya jumapili baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali
Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha
na inami za kishirikina.
Mkuu
wa kituo cha polisi cha Iyunga(kushoto) na Mwenyekiti wa kitongoji cha
Ikuti Bwana Emanuel Mwasote(katikati mwenye shati ya pink) wakijaribu
kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka
60(Pichani), kwa kumpeleka Kituo cha polisi Iyunga, baada ya wananchi
wenye hasira kali kuvamia kwenye nyumba yake na kutaka kuichoma moto
jana siku ya jumapili kabla ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali
Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha
na inami za kishirikina. Hata hivyo juhudi hizo ziligonga mwamba baada
ya wananchi hao kuwazidi nguvu polisi kutokana na Jeshi la polisi
kushindwa kufika mapema eneo la tukio na kuaanza kumdondoshea kichapo.
Bwana
Richard Mwakalinga akijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye
Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani),wakati wananchi wa
kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga jijini hapa kuanza kumdondoshea
kichapo jana siku ya jumapiliwakimtuhumu kujihusisha na inami za
kishirikina, wakati Jeshi la polisi halijafika eneo la tukio ili kuwedha
kuwadhibiti wananchi hao.
Wananchi
wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya,
wakimpiga kwa mawe Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka
60(Pichani), hapo jana siku ya jumapili wakimtuhumu kujihusisha na
inami za kishirikina.
Hapa
ni nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla
ya kuvunjwa na yeye akiwa ndani ya nyumba hiyo baada ya kutuhumiwa na
wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya
Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na imani za kishirikina.
Wananchi
wenye hasira kali wakivunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda
mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, baada ya kutuhumiwa na
wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya
Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
Wananchi
wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga,
jijini Mbeya wakimzingira Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa
miaka 60, kabla ya kumdondoshea kichapo wakimtuhumu kujihusisha na imani
za kishirikina.
Wananchi
wenye hasira kali wakiendelea kuvunja nyumba ya Mzee Asumwisye
Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, ambapo akina
mama nao hawakukaa nyumba kushiriki tukio hili, baada ya kutuhumiwa
na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata
ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
Baada
ya kupingwa Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana
siku ya jumapili, Jeshi la polisi lilifanikiwa kufika eneo la tukio
na kumchukua mzee huyo na kumpeleka Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini
Mbeya. Pichani ni baadhi ya askali na raia wema wakimuchukua mzee huyo
na kumpeleka kwenye gari la polisi kabla ya kumkimbiza hospitali.
Mke
wa Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, katikati
akilia kwa uchungu na kupewa msaada na wanawake wenzake, baada ya
mumewe kudondoshewa kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali
Kitongoji cha Ikuti, kata ya Iyunga jijini Mbeya jana siku ya jumapili
wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.(Picha na habari na
Ezekiel Kamanga)
HITIMISHO
Maoni
ya mtandao Jeshi la polisi linapaswa kufika kwa wakati muafaka mara
baada ya kupewa taarifa, lakini pia elimu itolewe kwa wananchi
kutojichukulia sheria mikononi kwani tuhuma na sio uthibitisho, kwani
mahakama pekee ndio ina mamlaka ya kutoa hukumu.
No comments:
Post a Comment