Pages

Tuesday, December 6, 2011

KILIMANJARO STARS YAISUKUMA NJE YA MASHINDANO MALAWI GOLI 1-0, YATINGA NUSU FAINALI


Mchezaji wa Kilimanjaro Stars Shomari Kapombe akichuana na Ndaziona Chatsalira wa timu ya Malawi katika mchezo wa robo fainali, katika michuano ya kombe la TUSKER CHALLENGE CUP 2011 uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, ambapo timu ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano hayo baada ya kuifunga Malawi goli1-0 katika kipindi cha Kwanza, lililofungwa na Nurdin Bakari kutoka wingi ya kulia. Leo Kilimanjaro Stars imeonyesha mchezo mzuri ukiacha makosa madogo madogo yaliyojitokeza, na kwa matokeo haya ambayo si makubwa sana, ni wazi kwamba wachezaji wa Kilimanjaro Stars bado wanahitaji kuongeza juhudi kwani michezo ya nusu fainali na fainali kwa vyovyote vile itakuwa ni migumu sana
Mchezaji wa Kilimanjaro Stars Mrisho Ngasa akishangilia goli pamoja na wachezaji wenzake, mara baada ya Nurdin Bakari kufunga goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza.
Wachezaji wakitoka nje mara baada ya filimbi ya mapumziko kupulizwa ikiashiria kuanza kwa kipindi cha lala salama.
Kikosi cha timu ya Malawi kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Malawi kikiwa katika picha ya pamoja.
Mashabiki wakishangilia wakati timu hizo zikicheza uwanjani

No comments:

Post a Comment