Askari wa Kikosi cha kuzima moto jijini Arusha wakijaribu kuzima moto huo bila mafanikio.
PICHA NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA
Moshi mkubwa ukiwa umetanda angani kutokana na moto huo.
Umati wa watu ukisangalia moto aliokuwa ukiunguza maduka jijini Arusha leo.
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-ARUSHA
WANANACHI wa jiji la
Arusha wameomba serikali kuongeza zaidi vifaa kwa kikosi cha zima moto ijini
hapa kwa kuwa mara nyingi sana
kikosi hicho kinashindwa kuokoa wananchi katika majanga ya moto kutokana na
kutokuwa na vifaa vya kutosha yakiwemo maji
Wakizungumza na Waandishi wa habari jijii hapa katika tukio la kuungua
kwa maduka tisa yaliyopo Stendi ya mkoa
katika mtaa wa majengo wananchi
hao walisema ukosefu wa maji ya kutosha kwa kikosi hicho unachanmgia
sana maafa na kwa hali hiyo Serikali inatakiwa kuliangalia hilo
Walisema kuwa mara nyingi sana kikosi hicho cha kuzima moto kinafima
kwa ajili ya kuokoa bidhaa pamoja na maisha ya watu ambao wamenusurika
na ajali za moto lakini wanashindwa kufanya kazi zao
Wananchi hao walifafanua kuwa endapo Kama
hali hiyo ya uzembe itaendelea basi kikosi hicho kitakuwa hakina faida kwa
wananchi, na hali hiyo inatakiwa kudhibitiwa mara moja kwa ajili ya kuokoa
maafa ya ajali za moto
Walisema kuwa katika tukio hilo la kungua kwa maduka kama
tisa ya biashara mbalimbali ambalo lilitokea majira ya saa tisa za mchana katika
mtaa wa majengo stendi kubwa
walisema kuwa magari yaliokuwa na maji
yalifika kwa muda muafaka lakini hawakuwa na maji ya kutosha
Wananchi hao walisema kuwa iwapo kama Magari hayo ya Fire
yangekuwa na maji ya kutosha basi ni wazi kuwa kwa kiwango kikubwa sana wangeweza kuokoa
maduka hayo dhidi ya moto mkubwa
Katika hatua nyingine Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Bw
Akili Mpwapwa alibitisha kuungua kwa maduka hayo tisa na kusema kuwa chanzo
bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea
No comments:
Post a Comment