Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, May 9, 2012

Angalia hapa jinsi basi la Muro lateketea kwa moto Morogoro



Basi la kampuni ya Kampuni ya  Muro Investment, T820BEY lillilokuwa klikitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku Mei 8,2012, haikusababisha madhara kwa abiria ispokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo.

 Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.

No comments:

Post a Comment