Hadija
Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma
Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo
za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa
kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012. Zifuatazo ni picha mbalimbali
za tukio hilo.
Pichani juuni Mkali
wa Bongo Fleva, Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum
ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika
Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Barnaba
Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani
hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye
uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Kilimanjaro.
DJ Choka akisugua vyombo kuendana na Roma Mkatoliki
Hapa ni usiku ....
...ni mchana
anastua...huyu ni Gwiji Hadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani hapo Ushirika. Mama alifunika mbaya katika show hii
Wakali
wa ragge kutoka kundi la Warriors from East la mjini Arusha
wakitumbuiza mashabiki katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music
Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Msanii
AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza show wake wakati wa
show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika
Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Hawa nao walikuwa wakitoa mpya ya kujirusha na kuangukia mgongo. Ni vijana wa Suma Lee.
Suma Lee akifanya vitu vyake jukwaani
Msanii
anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya
Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba
leo.
Nai Nai hapa ikiimbwa maana Omy Dimpoz alimshirikisha Ali Kiba
Wadau wakifuatilia show hiyo
Ali Kiba akienda sawa na vijana wake, hakika Moshi ilikuwa hapatoshi.
Gwiji la Muziki wa Taarabu nchini, na Mshindi wa Tuzo ya Mtumbuizaji
bora wa Kike, Hadija Kopa akifanya makamuzi katika tamasha maalum la
Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani
Kilimanjaro jana.
Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show
maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa
Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Chipukizi wa Bongo Fleva, anaetambulika kwa jina la Sungura akitumbiza
jukwaani, dogo huyu aliyeshinda katika shindano maalum la vipaji
atakwenda jijini Dar es Salaam kurekodi wimbo wake kwa DJ mkali wa Bongo
GWIJI la Taarab nchini Tanzania kutoka kundi la TOT, Hadija Omary
Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma
Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo
za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa
kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012.
Wasanii hao waliokuwa wakitumbuiza katika Tamasha maalum la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Licha ya hali ya hewa kuwa ya mvua na manyunyu ya hapa na pale wakati wote wa tamasha hilo lakini wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake jana walivunja rekodi ya Tamasha hilo kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo tofauti na mikoa mingine ya Dodoma na Mwanza ambako tayari Tanasha kama hilo limefanyika.
Kabla ya washindi wa Tuzo za Mziki za Kilimanjaro 2012 kupanda jukwaani walianza kupandaa chipoukuzi wa tatu wealio chuana vikali na mashabiki kumpitisha Msanii Sungura aliyeonekana kupagawisha vilivyo kwa wimbo wake wa Ndizi yangu.

Walianza jukwaani kupanda washindi wa Tuzo Bora ya Wimbo wa Ragge ambayo ilitwaliwa na kundi la Warriors from East waiotamba na vibao vyao kadhaa na kupiga jukwaani zaidi ya saa moja na kibao cha Arusha Gold kilichopawa tuzo kikiburudisha vilivyo na live show yao.
Mkongwe wa Taarab, Hadija Omary Kopa aliiudhihirishia umma wa wana Kilimanjaro kuwa yeye ni Mtumbuizaji bora wa Kike baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo zake kadhaa zilizojaa vijembe na mashairi ya ukweli ya taarab kutoka kundi lake la TOT huku uchezaji wake ukishangilia mwanzo hadi mwisho kwa jinsi alivyokuwa akiutikisa mwili wake.
Mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT nae alipanda jukwaani nyuma ya Hadija Kopa na kutoa burudani ya nguvu na wimbo wa Vifuu Utundu amabao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo na wanenguaji wake waili wa kike.
Akitanguliwa jukwaani na wacheza show wake machachari alikuwa ni mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Suma Lee aliyenyakua tuzo za wimbo bora wa Afro Pop kupiria kibao chake cha Hakunaga na Wimbo bora wa mwaka ambao pia ni hakunaga alikamua sawasawa.
No comments:
Post a Comment