Masaa machache baada ya kutoka Marekani
kuzungumza na wamiliki wa klabu ya Liverpool, leo kocha King Kenny
Dalglish ametimuliwa kazi ya ukocha pale Anfield.
Kenny Dalglish anaondoka Liverpool miezi
16 baada ya kuichukua timu hiyo baada ya kuondoka kwa kocha Roy Hodgson
mwezi January 2011. Dalglish ambaye ameiongoza Liverpool kubeba kombe
la Carling Cup msimu huu kabla hawajafungwa na kwenye fainali ya FA Cup
dhidi ya Chelsea.
Lakini kushika nafasi ya nane kwenye
premier league kulikuwa chini ya mategemeo ya wamiliki waliotumia kiasi
kingi cha pesa wakitegemea angalau kupata nafasi ya kushiriki kwenye
ligi ya mabingwa ya ulaya.
Habari kwa hisani ya shaffih blog
No comments:
Post a Comment