Pages

Friday, May 18, 2012

GWIJI WA DISKO DONNA SUMMER AAGA DUNIA



Disco legend ... Donna Summer


MALKIA wa Disco, Donna Summer amefariki dunia leo akiwa ana umri wa miaka 63 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa mwaka mzima.

Mshindi huyo wa tuzo tano za Grammy alikuwa mjini Florida wakati anafariki dunia.
Donna alijipatia umaarufu enzi 'majoka' miaka ya 1970 na alikuwa maarufu kutokana na vibao vilivyotikisa kama Love To Love You, I Feel Love na Hot Stuff - ambao ulitumika katika filamu ya The Full Monty.
Ameacha mume, mwimbaji na mtayarishaji Bruce Sudano, watoto wao wa kike Brooklyn na Amanda na mwingine wa Summer, Mimi, aliyempata katika mahusiano mengine.
Alizaliwa kwa jina la Donna Adrian Gaines mjini Boston, Massachusetts na muziki alianzia kanisani kwenye kwaya.
Mwalimu mama yake alisema alianza kuimba mara tu alipoanza kuzungumza. Mwishoni mwa miaka ya 1960, Donna alianzisha vikundi kadhaa vkabla ya kwenda Ujerumani kwa shughuli za kimuziki pia.
Kisha akasaini mkataba wa kurekodi na kutoa albamu yake ya kwanza, Lady of the Night mwaka 1974

No comments:

Post a Comment